• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HIFADHI ya Taifa ya Nyerere itakavyochochea utalii Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 28th, 2020

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Azimio la Bunge la kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Nyerere,   Novemba19, 2019 ambapo Rais Dkt.John Magufuli, aliweka sahihi kwenye Tangazo la kuanzisha rasmi Hifadhi hiyo.

Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ina ukubwa wa kilometa za mraba 30,893 na kuifanya kuwa moja ya hifadhi kubwa duniani yenye vivutio vingi vya asili na wanyamapori wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Nyerere  inayounganisha Mikoa minne ya Ruvuma, Pwani , Lindi na Morogoro.

Mndeme anasema Hifadhi hiyo imetokana na Pori la Akiba la Selous na kwamba Katika Mkoa wa Ruvuma hifadhi hiyo inapatikana katika wilaya za Namtumbo na Tunduru.

“Tunamshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais kwa kuanzisha hifadhi ya Nyerere ndani ya Mkoa wetu, itaenda kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi ndani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla’’,anasisitiza Mndeme.

Mndeme anabainisha zaidi kuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kuna wanyama wengi wakiwemo Simba, Tembo, Twiga, Chui, Nyati, mbwa mwitu na wengine wengi ambao ni vivutio vikubwa vya utalii.

Kulingana na Mndeme uwepo wa Hifadhi ya Taifa ya  Nyerere una faida nyingi katika Mkoa  wa Ruvuma ikiwemo Kufungua utalii katika ukanda wa kusini na hivyo kuchochea shughuli za utalii katika Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.

Faida nyingine za Hifadhi ya Taifa ya Nyerere anazitaja kuwa ni kutangaza vivutio vingine vya utalii vilivyopo ndani ya Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Mipaka ya nchi yetu yaTanzania na itasaidia katika kuongeza kipato cha  wananchi na Taifa kwa ujumla kutokana na shughuli za kitalii.

Anabainisha zaidi kuwa hifadhi hiyo,itasaidia katika kutangaza na kuongeza fursa za uwekezaji katika fukwe za Ziwa Nyasa kutokana na mwingiliano utakaokuwepo wa watalii wanaoingia na kutangaza vivutio vya Simba weupe na Tembo wakimbizi katika hifadhi ya Liparamba.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 28,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • SEKONDARI ya Dkt.Samia alama ya maendeleo Namtumbo

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.