Tanzania inajiandaa kushuhudia ukurasa mpya wa maendeleo! Tarehe 30 Julai 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atazindua rasmi mgodi mkubwa wa Uranium wenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.2! Katika wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Mgodi huu unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa.
Zaidi ya ajira 2,000 zinatarajiwa kutolewa moja kwa moja wakati wa utekelezaji wa mradi huu ikiwapa vijana na wananchi wa kawaida fursa ya kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo.
Hii ni hatua nyingine kubwa ya Tanzania kuelekea kuwa taifa la viwanda linalotumia rasilimali zake kwa manufaa ya watu wake.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.