Daktari wa mifugo Mkuu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dr. Solomon Nong’ona akizungumzia ugonjwa wa homa ya nguruwe katika Kanda hiyo, anasema Idadi ya nguruwe Tanzania ni karibu milioni 2.14 kati ya hao asilimia 90 wanafugwa na wakulima wadogo.
Dr.Nong’ona anasema wakulima hukosa njia sahihi za kuzuia magonjwa, elimu ya ufugaji na mipango bora ya kuzalisha nguruwe hao na kwamba ufugaji wa nguruwe katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini una vikwazo vingi na moja ya hivyo ni uwepo Homa ya nguruwe (ASF)
Abainisha zaidi kuwa homa ya nguruwe ni ugonjwa ulioanzia kwa mara ya kwanza katika Halmashauri ya Kyela katika mkoa wa Mbeya,Kutoka Novemba 2010 hadi sasa mwaka 2020 ugonjwa huo umeathiri karibu kila halmashauri zilizopo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
“Kuanzia Novemba 2019 hadi Machi 2020 mkoa wa Njombe ndiyo uliokuwa na matukio mengi kwenye Halmashauri za Makambako na Njombe ya homa ya nguruwe,Ugonjwa umeenea pia katika Mkoa wa Iringa kwenye Halmashauri za Kilolo, Mafinga na Mufindi’’,anasema Dr.Nong’ona.
Hata hivyo Daktari huyo wa Mifugo anasema,Februari 2011 Homa ya nguruwe imeendelea kutawanyika katika Halmashauri ya Nyasa kwenye ukanda wa Ziwa Nyasa mpaka katika Mkoa wa Ruvuma kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa,Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Anabainisha zaidi kuwa Machi 2011,ugonjwa wa homa ya nguruwe ulikuwa tayari umefika katika Halmashauri za wilaya za Chunya, Mbarali na Rungwe katika Mkoa wa Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kwenye Mkoa wa Songwe
Anasema asilimia 60 ya nguruwe waliopo nchini Tanzania wanatoka Nyanda za Juu Kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Songwe na Njombe
“Mradi wa nguruwe unaweza kuzalisha faida mpaka shilingi 252,165,100.00 (US$109,637.40) kwa mwaka katika nchi ,Wakati huo huo ugonjwa huu unaweza kusababisha hasara ya mpaka shilingi 2,094,922,800.00 (US$910,836.70) kwa mwaka katika nchi kwa hiyo mradi wa kufuga nguruwe ni benki inayotembea’’,anasisitiza Dr.Nong’ona.
Anasema mikoa ya Nyanda za Juu kusini ina Halmashauri 31 na kwamba ni halmashuari 14 tu ndizo hivi sasa zimeathirika sana na Homa ya nguruwe ambazo anazitaja kuwa ni Halmashauri ya Mji Makambako, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji Njombe.
Halmashauri nyingine anazitaja kuwa ni Mbarali, Chunya, Mbozi, Tunduma, Mufindi, Halmashauri ya Mji Mafinga,Halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Halmashauri ya Mji Mbinga, Halmashauri ya Ludewa,Halmashauri ya Songea na Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Februari 13,2020
Mbeya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.