HOSPITALI ya Kiuma inayomilikiwa na Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,imepokea msaada wa mashine ya X-Ray kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa uchunguzi magonjwa mbalimbali ikiwamo ya mionzi.
Mashine hiyo imetolewa na shirika la Neno na Tendo(Word&Deed)kutoka nchini Ujerumani ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa na ubora,katika Hospitali binafsi na Serikali kwa ukanda wa mikoa ya kusini.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt Nzelipa Masaga,wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro aliyeambatana na Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu na mwakilishi wa shirika la Word&Deed Susanna Diechmann.
Alisema,uhusiano uliopo kati ya Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi na Shirika hilo ndiyo uliowezesha kupatikana kwa mashine hiyo ya kisasa(Digital) ambayo imeanza kuwa msaada mkubwa watu wanaofika kupata huduma ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
DKT Nzelipa Masaga alisema,mashine hiyo ina uwezo wa kupima na kutambua kwa haraka magonjwa na shida nyingine katika mwilini tofauti na mashine iliyokuwepo zamani(Manual). Alisema, X-ray mpya ni suluhisho kubwa kwa watu wanaotoka maeneo mbalimbali hasa ikizingatia kuwa, Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imeipa Hospitali hiyo jukumu la kusimamia jumla ya zahanati tisa za vijiji jirani na kituo cha afya kimoja.
Alisema kuwa,kupatikana kwa mashine hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wagonjwa wanaofika kupata matibabu na wanaotakiwa kufanyiwa uchunguzi kwa njia ya mionzi.
Kwa mujibu wa Dkt Masaga,mashine hiyo ina uwezo wa kubaini matatizo ya wagonjwa wengi kwa wakati mmoja itasaidia kumaliza msongamano wa kusubiri vipimo kwa muda mrefu kwa watu wanaofika katika Hospitali.
Dkt Masaga alisema, kupatikana kwa mashine hiyo kunaashirikia mwanzo wa katika uboreshaji wa huduma za afya zinazotolewa na Kanisa hilo kwa kushirikiana na wadau shirika la Word&Deed kwani sasa wamefanikiwa hata kupanua huduma za matibabu ikiwamo ya mivunjiko(wanaopata ajali).
Dkt Masaga alifafanua kuwa,siku za nyuma walishindwa kutoa huduma ya uchunguzi kwa wagonjwa wengi kwa kuwa X-ray iliyokuwepo haikuwa na uwezo wa kutambua matatizo kwa haraka,hivyo baadhi ya wagonjwa walilazimika kwenda hadi Hospitali ya wilaya Tunduru mjini umbali wa km 67 kufuata huduma ya X-ray.
Hata hivyo alisema, changamoto kubwa ni upungufu mkubwa wa watumishi kwani mahitaji 105 na waliopo ni 56,na kuiomba serikali kutafuta njia ya kuwasaidia watumishi ambao wataongeza nguvu ya kuhudumia wananchi wanaofika katika Hospitali ya Kiuma.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la Word&Deed Susanna Diechmanna amehaidi kuwa, shirika hilo litaendelea kusaidia vifaa mbalimbali kwa Hospitali hiyo ili iweze kuboresha na kutoa huduma bor
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu ameripongeza shirika la Word&Deed kwa msaada huo, kwa sababu wananchi wa Jimbo la Tunduru kaskazini na mkoa wa Ruvuma wana uhakika wa kupata huduma ya mionzi karibu na haraka.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,licha ya kuwashukuru wafadhili hao kwa misaada mbalimbali wanayotoa kwa Kanisa la Upendo,amewataka wafanyakazi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.