Wananchi wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Wilaya, huduma ambazo hapo awali walilazimika kuzifuata nje ya Wilaya ya Tunduru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Chiza Marando amesema Hospitali ya Wilaya ya Tunduru imepata mabadiliko makubwa baada ya kukarabatiwa na kwamba Ukarabati huo umesaidia kuboresha huduma za afya na kuleta ahueni kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru.
Amesema wananchi wa Tunduru hivi sasa wanaweza kupata huduma bora za afya karibu na makazi yao.
Marando amesema serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 900 ambazo zimetumika kuboresha miundombinu ya hospitali, vifaa vya tiba, na mazingira kwa ujumla.
Amesema fedha hizo pia zimetumika kujengo jengo la wagonjwa wa nje (OPD),Maabara pamoja na ukarabati wa jengo la upasuaji .
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Hospitali ina vifaa vya kisasa vya tiba, na vifaa vya kufuatilia afya ya wagonjwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya wa Hospitali ya Tunduru, Dk.Wilfred Rwechungura amesema kukamilika kwa mradi huo kumepunguza changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu katika Hospitali na kurahisisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru.
Wananchi wamefurahishwa na juhudi za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.