SERIKALI ya Awamu ya Sita imetoa shilingi bilioni 1.2 ili kuboresha huduma za matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma .
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru Dr.Athuman Mkonoumo amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 900 zimetumika kukarabati miundombinu ya hospitali hiyo kongwe nchini iliyoanzishwa mwaka 1930.
Amesema serikali pia imetoa shilingi milioni 370 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura (EMD) na kwamba jengo limekamilika na kuanza kutoa huduma za dharura tangu Juni mwaka huu ambapo hadi sasa watu zaidi ya 86 wamepata huduma za EMD.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.