ALIYE kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Meja Jenerali Wilbert Ibuge amemkabidhi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas leo.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ibuge amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuteuliwa na Rais na kumshukuru kwa kumpa ushirikiano kipindi alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
“Nakushukuru sana kwa kunipa ushirikiano katika utendaji kazi kwa viongozi wote pamoja na watumishi wote wa Mkoa wa Ruvuma naomba muendelee hivyo nakufanya vizuri”.
Ibuge amesema uwepo wake Ruvuma kwa mda wa mwaka mmoja na miezi miwili na siku 14 alizotumika Ruvuma amejifunza vingi pamoja na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyoletwa na Rais pamoja na kusimamia Miradi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wa Ruvuma katika utendaji kazi.
“Nitumie fursa hii kuwa nitaanzia pale ambapo Ibuge ameishia sitakuwa na mapya zaidi ya kusimamia maendeleo ya Ruvuma”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza wananchi na watanzania kujiandaa kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi ifikapo Agosti 23,2022.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 6,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.