MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa kiasi cha shilingi Milioni Moja kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Lukimwa Wilaya ya Namtumbo.
Akizungumza katika ziara hiyo Ibuge amesema miezi mitatu iliyopita amekagua shughili za maendeleo katika sekta ya Elimu ikiwemo shule ya Lukimwa na hali haikuwa nzuri.
“Hali niliyoikuta haikunifurahisha katika muundo wa usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya fedha nyingi zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita”.
Ibuge amesema fedha zilizokuja kwaajili ya Miradi ila usimamizi wake uwe sahihi katika kamati za ujenzi ziundwe kwa usahihi na ununuzi ikiwemo na ushirikishwaji wa wananchi usilete mashaka.
Amesema Pamoja na jukumu la kumalizia miundombinu Maabara iliyojengwa ,zimekuja fedha za vyumba vitatu vya Madarasa Lukimwa za Maendeleo ya Taifa ya Uviko 19.
“Fedha hizo mkahakikishe zinajenga na kukamilika ifikapo Desemba 15,2021 washiriki na wasimamizi wajue zilipofikia “.
Hata hivyo amewapongeza wananchi wa Ligela kwa jitihada za kujenga Bweni kwa nguvu zao na mahitaji ya Miundo mbinu kwaajili ya wanafunzi wameonyesha jitihada naye akahamasika kuchangia ili wanafunzi waepuke kutembea umbali mrefu kufika shuleni.
Mkuu wa shule ya Sekondari Lukimwa Joachim Mapunda akisoma taarifa ya Shule hiyo amesema ufaulu wa wanafunzi umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka kwa kidato cha Nne ufaulu ulikuwa asilimia 89.2.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Novemba 9,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.