• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ILEJE wajifunza ukusanyaji mapato kupitia makaa ya mawe ya Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: May 26th, 2023

Viongozi na Wataalamu kutoka Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamefanya ziara ya mafunzo ya ukusanyaji mapato kupitia shughuli za uchimbaji makaa ya mawe katika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Wataalam hao kutoka Ileje wameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi. Farida Mgomi  na Menejimenti ya Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji Juma aliwaongoza wageni hao kutembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Kampuni ya Jitegemee Holdings uliopo Kijiji cha Ntunduwaro, Kata ya Ruanda pia wageni hao walitembelea katika eneo la kuchakata na kuuzia makaa ya mawe la Kampuni ya Jitegemee lililopo Kijiji cha Paradiso.

 Wataalamu hao pia walitembelea kituo cha ukaguzi na ukusanyaji wa mapato  kutokana na makaa ya  mawe katika bandari ya nchi kavu Kitai ambapo walijifunza namna Halmashauri hiyo inavyosimamia makusanyo ya ushuru, tozo na mapato mbalimbali yanayotokana na makaa ya mawe.

Biashara ya makaa ya mawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeleta mafanikio makubwa ambapo katika mgodi mmoja tu wa Jitegemee umeweza kutoa ajira za kudumu 85,ajira za muda 150 na serikali kuingiza mapato mbalimbali kutokana na ushuru na tozo mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kupata mafunzo hayo  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi kwa niaba ya  Menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Ileje  aliwashukuru viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga  kwa mafunzo  waliyopata katika ziara hiyo  ambayo amesisitiza  yataimarisha ukusanyaji wa ushuru na mapato kupitia sekta ya makaa ya mawe katika wilaya ya Ileje.

 

Biashara ya madini ya makaa ya mawe mkoani Ruvuma imeshamiri baada ya mauzo jumla ya makaa ya mawe ya  tani 450,675.32  ndani ya nchi na tani 1,060,699.05 ziliuzwa nje ya nchi katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2022.

 katika Mkoa wa Ruvuma,kuna jumla ya kampuni 14 za wachimbaji Makaa ya Mawe na kwamba katika Mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha Madini ya Makaa ya Mawe kilichouzwa ni jumla ya tani 639,482.55 ziliuzwa ndani ya nchi na tani 837,846.29 ziliuzwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Kwa kipindi cha hivi karibuni Mkoa wa Ruvuma umeweza kuvutia na kupata wawekezaji wengi waliowekeza kwenye shughuli zinazohusiana na madini ya Makaa ya Mawe kama Uchimbaji, Ununuzi, Usafirishaji na Uchenjuaji.

Mkoa wa Ruvuma una hazina ya makaa ya mawe zaidi ya tani milioni 227 ambayo yanatarajiwa kuchimbwa kwa miaka 300.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mei 25,2023

 

Matangazo

  • RATIBA ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 October 14, 2023
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara December 31, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAZIRI Mkuu katika Jubilei ya miaka 125 ya Jimbo kuu la Songea

    October 02, 2023
  • WAZIRI Mkuu awatahadharisha viongozi wa dini kuhusu uadilifu

    October 02, 2023
  • WAZIRI Mkuu alipongeza kanisa katoliki Jimbo Kuu la Songea kwa mafanikio ya kiroho na kimwili

    October 01, 2023
  • MKOA wa Ruvuma umefunguka,wananchi wa Msumbiji na Malawi wanapanda ndege Songea

    October 01, 2023
  • Tazama zote

Video

WAZIRI APONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA HALMASHAURI YA MADABA
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.