Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya, amempokea Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mheshimiwa Jaji James Karayemaha, katika kikao cha Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama kilichofanyika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo.
Jaji Karayemaha ameainisha jukumu kubwa la Kamati ya Maadili katika kuhakikisha maafisa wa mahakama wanazingatia maadili na kuimarisha heshima ya muhimili wa Mahakama.
Amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka maadili ya kazi.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Malenya amesisitiza umuhimu wa maadili bora kwa maafisa wa mahakama ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati na kwa usawa kwa wananchi wote.
Amehimiza ushirikiano kati ya wadau wa sekta ya sheria ili kuboresha mifumo ya utoaji wa haki nchini.
Kikao hicho kimejumuisha maafisa wa mahakama, viongozi wa serikali, na wadau wa sekta ya sheria, kikilenga kujadili maadili, uwajibikaji, na utoaji haki kwa ufanisi zaidi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.