• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

JENERALI Ibuge akabidhi ofisi kwa Kanali Laban

Imewekwa kuanzia tarehe: August 6th, 2022

ALIYEKUWA Mkuu wa mkoa wa Ruvuma  Meja Jenerali Wibert Ibuge,amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa huo Kanali Laban Thomas,makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa  na kushuhudiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Meja Jenerali Ibuge amempongeza Kanal Laban kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa na amemtakia majukumu mema Kanal Laban katika majukumu mapya ya nafasi hiyo.

Ibuge alisema kuwa, hana shaka  hata kidogo na mkuu huyo mpya kwa kuwa anaufahamu vyema mkoa wa Ruvuma wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Nyasa.

“nawashukuru wananchi,watendaji  na viongozi wote wa serikali ya mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano mlionipa wakati wote niliokuwa nanyi katika  nafasi ya mkuu wa mkoa kwa muda  wa  mwaka mmoja na miezi miwili, sina shaka na  Kanal Thomas  kwani ana uzoefu mkubwa na anaufahamu mkoa huu”alisema Jenerali Ibuge.

Alisema,akiwa mkoani Ruvuma kama kiongozi namba moja alifurahi sana kufanya kazi na wakuu wa wilaya ambao walimsaidia kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uaminifu mkubwa jambo lililosaidia mkoa huo kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Aidha Meja Jenerali Ibuge,amewashukuru waandishi wa Habari wa mkoa huo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandika na kutangaza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Alisema,vyombo vya Habari vilikuwa na mchango kubwa na kuwezesha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa iliyopiga hatua kubwa  ya kiuchumi na  kuwa miongoni mwa mikoa inayochangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa huo Kanal Laban Thomsa,amempongeza Meja Jenerali Ibuge kwa kupandishwa cheo kutoka Brigedia Jenerali hadi Meja Jenerali.

Amehaidi kutoa ushirikiano  kwa watendaji  na viongozi wa ngazi mbalimbali  za serikali katika mkoa huo huku akiwataka kwenda kusimamia  zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi huu nchini kote

“ naomba sana viongozi wenzangu kwenda kuhamasisha wananchi kujiandaa na zoezi la sensa ambalo ni muhimu kwa manufaa ya nchi yetu”alisema Kanal Laban.

“Jenerali Ibuge,nitaendelea kuomba ushirikiano wako,na kujifunza ubunifu wako katika majukumu ya kumsaidia  Mheshimiwa Rais kujenga nchi yetu”aliongeza Kanal Laban.

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema alisema,chini ya uongozi wa Jenerali Ibuge amejifunza mambo mengi mazuri ikiwamo suala la kujali muda kwa watumishi wa umma na usikivu kwa mtu yoyote bila kujali nafasi yake.

Alisema,tabia hiyo ni muhimu kwa kiongozi yoyote wa umma katika kuwatumikia wananchi.

Pia,amempongeza Jenerali Ibuge kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo kwa wananchi wa mkoa huo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.