Mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma upo katika hatua za umaliziaji na linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Oktoba mwaka huu.Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jimson Mhagama amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipofanya ziara ya kikazi kutembelea mradi huo kuwa serikali imetoa sjumla ya shilingi bilioni 3.3 kutekeleza mradu huo na kwamba hadi kukamilika jengo hilo linatarajia kutumia shilingi bilioni 3.8.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa jengo hilo ambapo amemuagiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi kwa asilimia 100 ili lianze kutumika rasmi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.