Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Mhagama, amekabidhi mashine za kupukuchua, kukoboa na kusaga nafaka zenye thamani ya Shilingi milioni 98 kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya kata na jumuiya zake, kwa lengo la kuimarisha uchumi wa chama hicho katika ngazi ya jamii.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya UWT Peramiho katika hafla fupi iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Komred Oddo Mwisho, alisema kuwa mashine hizo ni nyenzo muhimu zitakazochochea mabadiliko ya kiuchumi.
“Mashine hizi zitakuwa chachu katika kukuza kipato cha Chama ngazi ya kata na matawi, hatua itakayosaidia CCM kujitegemea zaidi kiuchumi,” alisema Mwisho.
Viongozi wa Chama waliopokea mashine hizo walieleza kuwa ni fursa adhimu ya kuimarisha mfuko wa Chama katika maeneo yao, huku wakiahidi kuzitunza na kuzitumia kwa tija ili ziweze kuwasaidia hata vizazi vijavyo.
Mbali na mashine hizo, Waziri Mhagama pia alikabidhi ng’ombe wa maziwa 16 wenye thamani ya Shilingi milioni 16 kwa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Jimbo la Peramiho, ikiwa ni juhudi za kuunga mkono uwezeshaji wa wanawake kiuchumi katika eneo hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.