KAMATI ya Maandalizi kuelekea siku ya kimataifa ya familia ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mchungaji Elimu Mwenzegule imedhamiria kuanza kutoa elimu rasmi kwa jamii kupitia majukwaa mbalimbali kuanzia Mei 6 hadi Mei 15 mwaka huu.
Kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia katika Mkoa wa Ruvuma kinatarajia kufanyika wilayani Namtumbo Mei 15 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.
Mchungaji Mwenzegule amesema Kamati hiyo katika mwezi huu inatarajia kutoa elimu kupitia redio za jamii,kutoa elimu kwa wanafunzi katika shule 16 za msingi na sekondari,kutoa elimu katika misikiti na makanisa na kutoa elimu kwenye mikusanyiko ya watu.
Kamati hiyo katika maadhimisho ya mwaka huu intarajia kutoa elimu kwa jamii kuhusu malezi chanya ya Watoto na familia kwa kuimarisha uelewa wa malezi na matunzo ya Watoto na wajibu wa wazazi na walezi katika malezi ya Watoto na familia.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia mwaka huu inasema “Tukubali tofauti zetu kwenye familia,kuimarisha malezi ya Watoto”.
Kaulimbiu hiyo inawahimiza wazazi na walezi umuhimu wa kumaliza tofauti zao,kudumisha upendo na amani katika familia kwa sababu mifarakano katika familia ina athari kubwa kwenye malezi na makuzi ya Watoto.
Taarifa ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum inaonesha kuwa katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024 jumla ya familia 14,600 zilitoa taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii kuwa na migogoro katika ndoa na mahusiano ya wenza.
Idadi hiyo ya taarifa ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya Pamoja kutoka katika jamii nzima ili kuleta mabadiliko na kupunguza changamoto za malezi na makuzi ya Watoto.
Baadhi ya wanakamati ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia Mkoa waa Ruvuma wakiwa kwenye kikao cha maandalizi kuelekea kilele maadhimisho hayo yanayoanzia Mei 6 hadi Mei 15 mwaka huu siku ya kilele
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.