• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMATI ya Bunge ya Mazingira yapongeza mradi wa mazingira ziwa Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: March 18th, 2024

WAJUMBE  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wamefanya ziara ya kutembelea Mradi wa Hifadhi Endelevu ya Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa (SLM-Nyasa) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga, wajumbe hao wamekagua moja ya boti za injini za uvuvi zilizotolewa kwa vikundi vya wavuvi katika Ziwa Nyasa ili kuwawezesha kujipatia kipato pasipo kuharibu mazingira.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kiswaga amesema kamati imeridhishwa na mradi huo na kuishukru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibu mradi huo ambao umeleta manufaa kwa wananchi na hifadhi ya mazingira.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis aliyeambatana na kamati hiyo ameendelea kuwahimiza wananchi kuitunza miradi hiyo.

Mradi wa SLM–Nyasa unalenga kuwajengea wananchi uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha maisha yao kwa kuwapa njia mbadala ya kujipatia kipato na hivyo kuachana na ukataji wa miti ovyo na uvuvi usio endelevu. 

Kupitia mradi huo Halmashauri ya Nyasa imefanikiwa kupanda miti takriban 3,500 rafiki kwa vyanzo vya maji, kupunguza ukataji holela wa miti kwa kutoa elimu ya matumizi ya majiko banifu yanayotumia kuni chache.

Mradi huo unatekelezwa katika halmashauri za wilaya zingine za Mbinga mkoani Ruvuma, Kyela  mkoani Mbeya , Ludewa na Makete mkoani Njombe  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.