• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMATI ya Siasa ya CCM Ruvuma yakagua chuo cha VETA Nyasa kinachogharimu bilioni mbili

Imewekwa kuanzia tarehe: July 1st, 2020


KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imekagua mradi wa ujenzi wa  chuo cha ufundi stadi VETA Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ambao unagharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyasa,Jimson Mhagama  amesema mradi unahusisha majengo 16 na kwamba fedha za mradi zimepokelewa kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza zimepokelewa zaidi ya bilioni moja.

Amesema mradi huo unatekelezwa  na mafundi mawili wakiwemo SUMA JKT ambaye anajenga majengo 14 na Simon Chiwanga ambaye anajenga vyumba viwili vya madarasa na kwamba mradi umetoa jumla ya ajira 123.

Mhagama amesema mradi huo unatekelezwa kwa kutumia mtindo wa force account ambapo wananchi kutoka Kata ya Kilosa ambako mradi unatekelezwa wanashiriki  na kwamba mradi ulianza Februari 21,2020 na unaarajiwa kukamilika Julai 31 mwaka huu.

Hata hivyo amesema mradi umefikia katika hatua tofauti za utekelezaji ambapo majengo saba yamefikia zaidi ya asilimia 80 ambayo ni nyumba ya Mkuu wa Chuo,kibanda cha mlinzi,vyumba viwili vya madarasa ,karakana na vyoo.

“Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kushirikiana na wananchi tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM kupitia mradi huu ambao utawanufaisha vijana wa Nyasa’’,alisisitiza Mhagama.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngeleja amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo ambao amesema utachochea wananchi kukiamini Chama Tawala kuendelea kutawala.

Hata hivyo Ngeleja ameushauri uongozi wa Halmashauri ya Nyasa kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na serikali kuhakikisha  inatangazwa na kufahamika kwa wananchi ili kutambua kazi nzuri zinazofanywa na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu  ya CCM Taifa Musa Homera ameipongeza Kampuni ya SUMA JKT kwa kutekeleza mradi huo  ambapo amesema wananchi wa Nyasa wameonesha moyo wa kujitolea katika utekelezaji wa mradi huo.

“Naomba serikali iendelee kuwaamini zaidi SUMA JKT kutokana na kutekeleza vema miradi ambayo mnapewa ,wilaya ya Nyasa inafanya vizuri katika utekelezaji miradi,inagawa,imezipita wilaya nyingine kongwe katika Mkoa wa Ruvuma’’,alisisitiza Homera.

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma inafanya ziara ya siku tano kupita katika wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma  kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 30,2020

Mbambabay

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.