• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMATI yaridhishwa na mradi wa maji Litisha Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: April 23rd, 2021

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Odo Mwisho imekagua mradi wa maji Litisha wilayani Songea na kuridhishwa na mradi huo.

Wanachi wa Kata ya Litisha wameanza kunufaika na huduma ya mradi wa maji, ulioanza kutekelezwa m Mei 29 ,2020 na  unatarajia kukamilika Juni 30,2021

Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji taka na usafi wa mazingira Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa amesema mradi huo ulisanifiwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 473,mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 70.

Mhandisi Kibasa amesema ujenzi wa mradi huo ni wa kisima chenye urefu wa mita 181 na kina uwezo wa kuzalisha maji lita 9,000 kwa saa ambapo amesema kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wakazi 3,226 wa kata ya Litisha.Ameitaja miradi mingine ya maji inatarajiwa kujengwa  katika Vijiji vya Litowa,Peramiho (B) na Nakahuga Halmashauri ya Wilaya ya Songea kupitia mfuko wa maji wa Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji Litisha Saidi Hashimu kwa niaba ya wananchi ameishukuru Serikali kwa kuwajengea mradi huo ambao amesema unakwenda kutatua changamoto maji zilizowakabili kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ametoa wito kwa wananchi kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji kwa makusudi kwani kitendo hicho kinawakosesha wananchi kupata huduma ya maji.

Mwisho ametoa rai kwa wananchi kulinda vyanzo vya maji na kupanda miti rafiki ya maji ambayo itasaidia vyanzo hivyo kuwa endelevu.

Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema hatamfumbia macho mtu yoyote atakayethubutu kuharibu na kuhujumu miundo mbinu ya maji kwa sababu Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miradi ya maji,hivyo lazima miradi hiyo ilindwe na kutunzwa.

Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Ruvuma imemaliza ziara ya siku tatu kukagua miradi ya maji katika wilaya za Songea na Namtumbo.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 24,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.