• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMBI ya matibabu ya kibingwa ya afya ya akili kufanyika Ruvuma kwa siku tano

Imewekwa kuanzia tarehe: December 18th, 2024

MADAKTARI Bingwa wa  kambi ya matibabu ya kibingwa ya afya ya akili wanatoa huduma za matatibu  kwa siku tano kuanzia Desemba 16 hadi 20 mwaka huu.

Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kambi hiyo  katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea,alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano.

Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mbano ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuhakikisha huduma za afya ya akili zinatolewa kwa wananchi.

“Nimefurahishwa na juhudi za kutoa huduma za  matibabu ya afya ya akili. Idadi ya wagonjwa wa nje na wale wa kulazwa mnaowahudumia inaonesha kuwa hitaji la huduma hizi ni kubwa, hasa kwa magonjwa yanayoongoza kama vile msongo wa mawazo,( Schizopherenia ) na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya’’,alisema.

Amesema Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia Wizara ya Afya imeweka kipaumbele cha tisa  Katika kuimarisha huduma za afya ya akili.

Hata hivyo amelitaja lengo ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi, bila kujali mazingira yake, anapata huduma bora ya afya ya akili na kwamba huduma tembezi ni moja ya mikakati  madhubuti inayolenga kufanikisha azma hiyo.

Amesisitiza kuwa madaktari Bingwa ya afya ya akili waliopo mkoani Ruvuma hawatasaidia tu kutoa huduma kwa wagonjwa, bali pia wataongeza maarifa kwa watoa huduma kupitia mafunzo na kubadilishana uzoefu.

 

Ametoa wito kwa watoa huduma wote kuendelea kuwa na moyo wa kujituma, kujifunza, na kushirikiana kwa ukaribu na madaktari bingwa  wa afya ya akili.

Naye Daktari Bingwa wa Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Taifa Dodoma Dr. Sadiki Mandaru amesema hii ni kambi ya pili kufanyika  mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo kambi ya kwanza ilifanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Ametaja moja ya uchunguzi wa afya ya akili ambao utapewa kipaumbele ni Pamoja na  uchunguzi  wa  Sonona, wasiwasi uliopitiliza, matumizi ya dawa za kulevya,na kutoa ushauri wa kisaikolojia, na kimatibabu.

Amesema madaktari bingwa hao pia watafanya  kipimo kikubwa cha umeme wa ubongo  ambacho ni maalum kwa watu wenye ugonjwa wa kifafa.

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dr. Magafu Majura, amewashukuru Madaktari bingwa wa afya akili kwa ujio ambao wamesema watasaidia kutoa matibabu kwa watu wenye changamoto za afya ya akili.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.