• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMPENI ya kutokomeza kifua kikuu Tunduru inavyopunguza maambukizi mapya

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2023

WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na kitengo cha kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,imeendelea na kampeni ya upimaji  wa maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa wananchi katika maeneo ya vijijini wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Masonya wakati wa kampeni za uelimishaji,uibuaji na uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu, Muhudumu wa afya ngazi ya jamii Menrad Hyera alisema,lengo la kampeni hizo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa salama bila maambukizi ya ugonjwa huo unaotajwa kuwa miongoni mwa magonjwa kumi yanayopoteza watu wengi hapa nchini.

Alisema,kutokana na ukubwa wa tatizo la kifua kikuu hapa nchini, ndiyo maana serikali  ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau Shirika la Amref Health Africa na DMH wanaendelea na mapambano ya kutokomeza ugonjwa huo ili jamii iwe salama na kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Alisema,ugonjwa wa kifua kikuu unatibika na huduma zake zinatolewa bure katika vituo vyote vya kutolea huduma,Hospitali  binafsi na serikali hapa nchini na kuwataka wananchi kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi  wa afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wameambukizwa TB.

Ametaja dalili za kifua kikuu  kwa watu wazima ni kupungua uzito,kutokwa na jasho jingi nyakati za usiku,kukohoa zaidi ya wiki mbili,kukohoa makohozi yaliyochanganyika na damu na kwa watoto kulilia,kukosa raha na makuzi duni.

Amewaonya wananchi,kuacha tabia ya kumeza dawa bila kupata ushauri wa kitaalam au kukimbilia kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala kila wanapohisi kuwa na homa,badala yake kwenda katika  vituo vya kutolea huduma ili kufanya uchunguzi wa afya zao.

Hyera,amewashauri kufuata na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wakiwemo wahudumu ngazi ya jamii wanaopatikana katika maeneo yao ili kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua kikuu.

Hyera ameitaka jamii, kuwa na mahusiano ya karibu na wahudumu wa  afya ngazi ya jamii waliopo katika maeneo yao wenye jukumu la kukusanya sampuli za makohozi na kuzipeleke kwenye vituo  vya kutolea huduma na Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

Kwa upande wake Mratibu na mdhibiti wa kifua kikuu kutoka shirika la Amref-Health Africa Lilian Ishengoma alisema,lengo la kampeni hiyo ni kuwafikia wagonjwa wote waliopo katika jamii ili kuwaanzishia matibabu na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Ishengoma,amepongeza jitihada zinazofanywa na Hospitali ya wilaya ya Tunduru kitengo cha kifua kikuu na ukoma kwa kazi nzuri katika  kutokomeza  ugonjwa huo na kutaka maeneo mengine kuiga ili kwa pamoja nchi yetu ibaki salama bila maambukizi ya kifua kikuu.

Mkazi wa kijiji cha Masonya Ahmad Halfani,ameishukuru serikali kwa kufanya kampeni hizo kwani zinasaidia sana wananchi kupata uelewa kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma na kufanya uchunguzi na kufahamu hali za afya zao.

Hata hivyo,ameiomba Serikali kuendelea kufanya kampeni  hizo  mara kwa mara ili kuwafikia watu wengi, kwani ugonjwa wa kifua kikuu upo na watu wengi wanaugua bila kupata tiba sahihi jambo lililochangia baadhi ya familia kukosa nguvu kazi na kukabiliwa na umaskini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.