Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid , imefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali tangu kutekelezwa kwake katika mikoa 17 nchini, ambapo imemnusuru binti alietaka kuozeshwa na wazazi wake Mara baada ya kuhitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza, imeelezwa kuwa binti huyo anatarajiwa kuhitimu kidato cha sita mwaka huu 2025.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Damas Ndumbaro, ameeleza kuwa kupitia kampeni hiyo walibaini uwepo wa taarifa ya binti aliehitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza Mkoani Shinyanga kutaka kuozeshwa na wazazi wake, hivyo walifanya ufuatiliaji kwa kufika katika harusi hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria ambapo binti alifanikiwa kuendelea na masomo ikiwa mwaka huu anatarajiwa kuhitimu kidato cha sita.
Ameeleza kuwa Katika utekelezaji wa kampeni hiyo wamejikita katika utoaji wa elimu ya sheria ili watanzania wapate ufahamu pamoja na utatuzi wa migogoro mbalimbali inayowakabili hususani wanyonge wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa nchi ndio maana wamekuwa msaada mkubwa kwao kwani kampeni hiyo ni utekelezaji wa Mpango wa Rais Samia Suluhu Hassani.
Amesema kampeni hiyo imejikita katika utoaji elimu juu ya masuala ya uraia na utawala bora kwa kushirikiana na Asasi za kiraia, Chama cha Mawakili Tanganyika, pamoja na madawati ya maendeleo ya jamii katika kila Wilaya ili kuhakikisha kampeni hii inakuwa endelevu, kwani inatekelezwa kwa kufuata 4R za Rais Samia Suluhu Hassan, ambazo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na kujenga upya.
Hadi hivi sasa jumla ya mikoa 17 imekwisha fikiwa na kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia huku akiitaja mikoa mitano inayotarajiwa kufikiwa mapema mwezi huu ambayo ni Mwanza, Lindi, Pwani, Rukwa na Mbeya
Kampeni hiyo inatekelezwa chini ya kauli mbiu isemayo "Msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo", kwani jamii ikikosa amani hakuna maendeleo, badala ya mwananchi kumtafuta mwanasheria kwasasa mwanasheria ndio anamtafuta mwananchi, hadi hivi Sasa zaidi ya watu milioni 1 na laki 3 wamefikiwa na kampeni hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.