Juhudi za kuhamisisha Wawekezaji katika Kilimo zimeendelea kuwanufaisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla ambapo hadi kufikia mwaka 2020 yapo Makampuni mawili makubwa yaliyowekeza katika Kilimo kama ifuatavyo;
Kampuni ya AVIV; Kampuni hii inajihusisha na kilimo cha zao la Kahawa, hadi kufikia mwaka 2020 jumla ya hekta 1,025 zimelimwa na kupelekea kuongeza ajira toka 1,000 mwaka 2015 hadi 3,000 mwaka 2020.
Kampuni ya Siliverland (Shamba la Ndolela); inajihusisha na kilimo cha mazao ya Mahindi, Maharage, Ngano, Parachichi, Soya na Shayiri, hadi kufikia mwaka 2020 jumla ya hekta 1,200 zimelimwa na kupelekea kuongeza ajira ya jumla ya watu 1260 hadi kufikia mwaka 2020. Mwekezaji huyu pia ameweza kujenga Vihenge 8 (Silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 16,000 za mazao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.