Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), amekagua Uwanja wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 uliopo jijini Mbeya na amewakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika Maonesho hayo katika Kanda zote ili kuweza kujifunza teknolojia mbalimbali zitazowanufaisha wakulima na wazalisha wa bidhaa za kilimo.
Maonesho ya Nane Nane 2024 yatakuwa katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere; Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi; Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.