Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Steven Ndaki amehimiza ukamilishaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Ndaki amesema hayo alipotembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya Songea hivi karibuni.
Ndaki amesema ameridhishwa na ujenzi wa miradi inayoendelea kujengwa pia amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na kuagiza dosari ndogo ndogo zirekebishwe.
“Jitihada iongezwe ili miradi yote ikamilike na ianze kutoa huduma kwa wananchi”,alisema Ndaki.
Ametoa rai kwa wananchi kuanza kupata matibabu katika Hosptali ya Wilaya ya Mpitimbi ambayo imeanza kutoa huduma hiyo kuanzia Julai 15 mwaka huu.
Ameagiza katika ujenzi wa miradi ya maendeleo inyotekelezwa ndani ya mkoa kwa njia ya force akaunti suala la uzalendo ni muhumu likapewa kipaumbele kwasababu linalinda maslahi na uaminifu katika ujenzi na utekelezaji wa mradi husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Bulenganija ameishukuru timu ya ukaguzi kwa kukagua miradi na kutoa mapendekezo ambayo yanasaidia kuboresha ujenzi wa miradi hiyo.
Bulenganija amesema jitihada za ukamilishaji wa miradi zitaongezwa na miradi itakamilika na kuanza kutoa huduma kama lengo la serikali linavyoelekeza la utoaji huduma kwa wananchi hasa wanyonge.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma katika ziara hiyo amekagua Jumla ya miradi nane ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha Matimira, Magagura,Hosptali ya Wilaya iliyopo Mpitimbi na miradi mitano ya ujenzi wa vyoo bora (SWASH) vinavyojengwa katika shule za Msingi Mpitimbi, Mkurumusi,Peramiho ,Mapinduzi na Humbaro.
Imeandikwa na
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI SONGEA DC.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.