KATIBU Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Sefu Madenge ametoa rai kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia.
Madenge ametoa rai hiyo wakati anazungumza na watumishi hao katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,lengo kubwa la kikao hicho likiwa ni kujitambulisha rasmi kwa watumishi hao baada ya kuhamia Mkoa wa Ruvuma akitokea Mkoa wa Dar es salaam.
Katibu Tawala huyo amewaasa watumishi hao kufanya kazi kwa Pamoja kama timu,kupendana kwa dhati,kusaidiana na kuelewana ili kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
“Kila mmoja afanye kazi kulingana na fani yake, fanyeni kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu,busara na kuzingatia misingi ya utumishi wa umma ikiwemo uwajibikaji’’,alisisitiza Madenge.
Madenge amesisitiza kuimarisha usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa wa Ruvuma na kusimamia sekta ya elimu ambayo haifanyi vema katika Mkoa wa Ruvuma.
Hata hivyo Katibu Tawala huyo ameagiza kuboreshwa kwa mazingira katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuimarisha usafi katika viunga vya mji wa Songea hali ambayo itavutia watu wengi.
Awali akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu Katibu Tawala Msaidizi ,Rasilimali watu Mkoa wa Ruvuma Salum Kateula amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa ina jumla ya watumishi 174 ambao baadhi yao wanafanya kazi katika ofisi za wakuu wa wilaya tano zilizopo mkoani Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.