Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amewataka wauguzi na wakunga kujitoa na kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Ametoa wito huo wakati akifungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wauguzi (TANNA) Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage mjini Songea.
"Kazi yenu sio rahisi, lakini mtumainie Mungu, mfanye kwa bidii, mjitume, muwe wazalendo, muwapende hao wagonjwa mtaokoa maisha, kazi yenu ni ngumu mnahitaji kujitoa," alisema Makondo
Ameongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa majukumu wanayotekeleza ya kuangalia wagonjwa ambapo changamoto zinafanyiwa kazi na Serikali, hivyo wawe tayari na kujitoa kuwahudumia wagonjwa.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, amesema kuwa Wauguzi ni nguzo ambayo inabeba majukumu yote katika mzigo wa kuwatunza wagonjwa.
Amesema kama ilivyo kauli mbiu ya Kongamano lao inayosema "Wauguzi Sauti Inayoongoza, Wekeza katika Uuguzi, Heshimu Haki, Linda Afya" Wauguzi hao wamekuwa wakiitekeleza ipasavyo kwa kulinda afya na kuheshimu haki.
Malengo ya Kongamano hilo la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha wauguzi (TANNA) Mkoa wa Ruvuma ni kuhimizana katika umoja na kujitoa katika kuwahudumia wagonjwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.