Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amezinduza duka jipya la Vodacom lililopo mtaa wa Mtini katika Manispaa ya Songea.
"Duka hili limekuwa mkoani Ruvuma tangu mwaka 2008 ni dhahiri kuwa wananchi wamekuwa wakinufaika na huduma hizi wakati wote, nichukue nafasi hii kuwapongeza viongozi wa kampuni ya Vodacom, kitaifa na kimataifa huduma zenu zimeendelea kuboreshwa, pia katika uzinduzi huu tunashuhudia huduma zilizoboreshwa zikiwemo bima kwa vyombo vya moto na afya," alisema Makondo
Ameongeza kuwa kwa huduma hizo zilizoboreshwa kampuni imefanikiwa kuwafikia wananchi na kuendelea kuboresha huduma zao za kiuchumi na kijamii na kuwasisitiza kuzingatia usalama wa wateja katika usajili wa laini za simu na kuhakikisha wateja wanaendelea kufurahia huduma zao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo akizungumza kwenye uzinduzi wa Duka la Vodacom mjini Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.