Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba, amewaagiza watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule wote kuhakikisha kila Mzazi anachangia gharama za chakula ili kumhakikishia mtoto kupata chakula .
Mwampamba ameyasema hayo katika kikao cha Kamati ya Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea yaliyopo Lundusi Songea.
Kikao hicho ambacho huratibiwa na Divisheni ya Afya, kimeshirikisha watendaji wa kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Katibu Tawala huyo amewaagiza watendaji wa Kata na Kijiji kuhakikisha wazazi wote wanachanga chakula kwa ajili ya Watoto wao.
Amesisitiza elimu ya lishe bora na ulaji iendelee kutolewa kwa jamii kupitia Mikutano yote ya Hadhara, Makongamano, Semina na Mashuleni pamoja na kupitia vyombo vya Habari.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.