• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAYA 115 Songea zapata msaada wa umeme jua

Imewekwa kuanzia tarehe: August 16th, 2022

SHIRIKA la Children of Songea kwa kushirikiana na wadau  wengine shirika la Africa Power na Kuwasolar,wametoa msaada wa umeme jua(solar)kwa kaya 115 zinazoishi  mazingira magumu katika kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa miradi wa shirika hilo Shaban Tindwa alisema,kwa muda mrefu wanatoa misaada kwa watu na familia zinazoishi katika mazingira magumu  ili kuwafariji  kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali  za kimaisha.

Alisema, gharama za solar hizo ni  zaidi ya Sh.milioni 18 na mpango wa shirika  la Children of Songea ni kuwasaidia watoto hao ili wapate nafasi kubwa ya kusoma na hatimaye waweze kutimiza malengo yao.

Alisema, kwa mara ya kwanza wameanza kutekeleza mpango huo katika kata ya Ruvuma, na wamelenga hasa kaya zenye watoto wanaosoma shule za msingi na sekondari.

Tindwa alieleza, matumaini yao kuwa solar hizo zitawasaidia watoto wanaotoka kwenye kaya hizo kuongeza taaluma kwenye masomo yao  kwa kupata muda mwingi wa kujisomea hasa nyakati za usiku.

Alisema,tangu mwaka 2015 Children of Songea inatoa vifaa vya shule,sale kwa wanafunzi,chandarua kwa watoto ili kuwakinga na ugonjwa wa malaria,kulipia bima ya Afya(CHF)  kwa watoto wanaotoka kwenye kaya zinazoishi mazingira magumu na kukarabati nyumba.

Aidha alisema, kupitia mpango huo wamefanikiwa sana kuongeza hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kufanya vizuri darasani na hatimaye kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika shule mbalimbali hapa nchini.

Mwakilishiri wa KuwaSolar Najumo Kipepe alisema,lengo la msaada huo ni kusaidia kupata mwanga ambao utasaidia kuchagiza taaluma kwa wanafunzi na kujikwamua kiuchumi katika kaya hizo.

Kipepe, amewataka wazazi na walezi wa watoto hao kuhakikisha wanatunza solar hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na zisaidie kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili.

“ni furaha yetu kuona kila mmoja nafikiwa na umeme popote alipo kwa kuzingatia  hasa umuhimu waw a umeme kwenye makazi yetu”alisema Kipepe.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la Africa Power Richard Wallec alisema,mara ya kwanza alipotembelea baadhi ya kaya hizo aliumizwa sana kuona hakuna mwanga wa kutosha kwenye nyumba zao licha ya kuwa  ilikuwa majira ya mchana.

Richard,amewashukuru wakazi hao kwa kumkaribisha katika jamii yao  hali iliyomwezesha kufahamu baadhi ya changamoto na matatizo yanayowakabili na kuhaidi  kuendelea kuzisaidia familia hizo.

Mmoja wa wazazi Pilmina Hyera,ameyashukuru mashirika hao kwa msaada huo na kueleza kuwa, solar hizo zitawasaidia watoto wao kusoma nyakati  za usiku na kuhaidi kama wazazi watahakikisha wanawasimamia watoto wao kusoma kwa bidi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.