Kaya 1498 zimechaguliwa Mkoani Ruvuma kwa ajili ya Sensa ya kilimo,Uvuvi,na Ufugaji ambayo inafanyika kwa siku 60 kuanzia Agosti 5 hadi Oktoba 3 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngai wakati anazungumza baada ya kukagua zoezi la sense hiyo katika kijiji cha Mbingamhalule wilayani Songea.
Ngai amesema zinahitaji Takwimu rasmi zinazopatikana kupitia mazoezi kama hayo zinazowezesha kujua kwenye changamoto mbalimbali katika sekta za kilimo,mifugo na uvuvi.
“Serikali inatakiwa kupata Takwimu sahihi inapoandaa mipango yake katika sekta isiwe na takwimu za kufikilika bali iwe na takwimu rasmi kupitia sheria ya 2015 inatoa majukumu kwa wadau wanao hojiwa,na waandishi wa habari na vyombo vyao’’,alisema.
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Ruvuma Mwantumu Uhenga amesema zoezi hilo kinafanyika katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma na kwamba hii ni mara ya tano kufanyika sensa ya kilimo,mifugo na uvuvi ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika ,mwaka 1974.
Uhenga amesema kutakuwa na madodoso matatu ambayo ni dodoso la wakulima wadogo,wakulima wakubwa na dodoso la jamii.
Afisa mahusiano ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Ameir amesema sensa ya kilimo,Uvuvi,na Ufugaji inafanyika ili kutekeleza maendeleo ya nchi yetu ili kupata takwimu sahihi na mipango sahihi na kwamba matokeo ya sensa hiyo ni muhimu kwa mwananchi .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa
31 Agosti 2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.