Jumla ya kaya 18,912 zimehitimu mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge wakati anazungumza kwenye kikao kazi cha waratibu,wahasibu na maafisa ufuatiliaji wa TASAF Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mipango ofisi ya
Mkuu wa Mkoa mjini Songea.
Amesema hadi kufikia Juni 2024 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na Jumla ya kaya 65,089 za walengwa wa TASAF katika vijiji 685.
Hata hivyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma amezitaja kaya ambazo zitaendelea na mpango wa TASAF katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni kaya 46,177.
“Serikali imeridhishwa na matokeo hayo kwa kuwa Katika utekelezaji wa shughuli yeyote ya maendeleo inategemea kuona mafanikio na lengo kuu la mpango huu ni kuziwezesha kaya masikini sana kuongeza kipato,fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu’’,alisisitiza.
Madenge amebainisha kuwa TASAF imewezesha fedha za kutosha kwa jamii ambapo ametoa rai kwa wadau kusimamia vya kutosha fedha hizo na kuhakikisha zinaleta tija kwa jamii.
Katibu Tawala huyo amewaagiza waratibu wa TASAF kufuata taratibu za manunuzi wakati wa utekelezaji wa shughuli za mpango hususan kutumia mfumo wa manunuzi wa NeST kwa manunuzi na mahitaji ya ofisi na mwongozo wa manunuzi ngazi ya jamii utumike ipasavyo.
Maagizo mengine aliyoagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma ni kila Halmashauri kutoa taarifa mapema kwa walengwa ili kuepuka fedha nyingi kurudishwa TASAF Makao makuu wakati wahusika hawapo na magari ya mradi wa TASAF yatumike katika kazi za mradi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF kutoka Makao makuu Lazaro Mapimo akizungumza kwenye kikao kazi hicho amewaagiza waratibu hao kuhakikisha kuwa wanafuata miongozo na kanuni za kiutumishi kwa kuwa TASAF ni mradi wa serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.