• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAYA masikini Songea zapigwa jeki

Imewekwa kuanzia tarehe: September 3rd, 2022

KAYA zipatazo 110  zinazoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi katika kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea,zimepatiwa msaada wa vifaa vya kufukuza  mbu majumbani (Mosquito fans) sambamba na kupatiwa elimu  kuhusu matumizi sahihi ya vifaa hivyo na chandarua.

Vifaa hivyo, vimetolewa na kampuni ya Afrika Power kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Children of Songea kwa ajili  ya kuwakinga wananchi hasa watoto wadogo wanaishi kwenye mazingira magumu  dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo,mwakilishi wa kampuni ya  Afrika Power ya  Dar es slaam Najumo Kipepe alisema,suala la afya ni muhimu na  wameamua kugawa vifaa hivyo ili wananchi wavitumie katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria ambao unatajwa kuwa miongoni mwa magonjwa yanayopoteza maisha ya watu wengi hapa nchini.

Kipepe alisema,kampuni ya Afrika Power inajali na kuthamini sana eneo la afya  za wananchi ndiyo maana imetoa vifaa kwa kutambua kuwa kata ya Ruvuma ni miongoni mwa maeneo yenye idadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na yako katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Kipepe,vifaa vina thamani ya Sh.milioni tano na ni mwendelezo wa kampuni hiyo kutoa misaada mbalimbali kwa jamii  hasa yenye mahitaji maalum wakiwamo watoto wanaosoma kwenye shule za msingi na sekondari.
Aliongeza kuwa, mwezi uliopita walitoa msaada wa  umeme jua(solar)ili kuwawezesha watoto kupata muda wa kujisomea hata nyakati za usiku na waweze kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.
“kwa hiyo tumekuja kata ya Ruvuma mkoani Ruvuma kugawa vifaa hivi ili visaidie jamii ya apa hasa wanafunzi ili kuimarisha afya zao na kuhakikisha jamii yote inakuwa na afya njema kwa kuepukana na malaria”alisema Kipepe.

Alisema,kazi kubwa inayofanyika ni kuunga mkono juhudi mbalimbali za serikali katika kutokomeza maradhi mbalimbali na wanafunzi wanapata nafasi na muda wa kujisomea ili waweze kufanya vizuri katika safari yao ya masomo.

Mwakilishi wa Shirika la Children of Songea Ester Zenda alisema,kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo ni kusaidia  watu wanaoishi katika mazingira magumu na watoto yatima katika Manispaa ya Songea.
Alisema,awali walipofika kwa mara ya kwanza walielezwa kuhusu ukubwa wa tatizo la ugonjwa huo katika kata ya Ruvuma ambapo  kwa kushirikiana na serikali za mitaa wamefanikiwa kupata angalau watoto 110, hata hivyo wanashindwa kuwafikia watu wote kutokana na kuwepo kwa watu wengi wanaohitaji msaada.Alisema,wamelipia  gharama za matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF)ili watoto  hao wawe na uhakika wa kupata matibabu pindi wanapougua na kuwaomba wadau wengine kujitokeza na kuungana nao ili kwa pamoja  waweze kuwasaidia watu wenye mahitaji.
Naye muhudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka kata ya Ruvuma Asia Milanzi alisema, ni vyema jamii ikakumbuka kutumia  chandarua mara kwa mara  wakati wa kulala ili kupata ugonjwa wa malaria ambao ni tishio kwa jamii nyingi za Kitanzania.
Amewahimiza kuhakikisha wanakula vyakula bora ili kuepuka uwezekano wa kupata na ugonjwa huo ambao unachangia kwa kiwango kikubwa tatizo la umaskini.
Alisema,kwa kawaida mtu anayeugua malaria na magonjwa mengine  kuna uwezekano mkubwa wa kuleta umaskini ndani ya familia kwa sababu hana uwezo wa kufanya kazi za kuleta kipato.
Alisema,kama muhudumu wa afya ngazi ya jamii atahakikisha wananchi wa eneo hilo wanaendelea kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya vyandarua  ili wasipate malaria na kuathiri afya zao.
Afisa Mtendaji wa kata ya Ruvuma Beatrice Kapinga amelishukuru shirika la Children of Songea kufika katika kata hiyo na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wanaotoka katika kata hiyo ambayo itasaidia kujikinga na maradhi mbalimbali na kupata muda wa kujisomea.
Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake Salkha Njelekela mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Matogoro alisema,vifaa hivyo vitawasaidia kujikinga na ugonjwa wa malaria na kuongeza hamasa ya kujisomea hasa nyakati za usiku.
MWISHO.













ReplyReply allForward






Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.