Novemba 14, 2022 wanafunzi Kidato cha Nne na Maarifa nchini kote wataanza Mtihani wa Kitaifa utakaofanyika katika jumla ya shule 5,212 na Vituo vya Mitihani vya Watahiniwa wa Kujitegemea au Faragha 1,794.
Kwa upande wa Mtihani wa Kidato cha Nne, jumla ya watahiniwa 566,840 wamesajiliwa kufanya Mtihani huu ambapo kati yao Watahiniwa wa Shule ni 535,001 wavulana wakiwa 247,131 sawa na asilimia 46.19 na wasichana 287,870 sawa na asilimia 53.81 ya watahiniwa wote wa shule.
Aidha, watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 852 kati yao 480 ni wenye uoni hafifu, 62 ni wasioona, 19 ni viziwi, 152 ni wenye mtindio wa akili na 139 ni wenye ulemavu wa viungo.
Kwa Mwaka 2021 idadi ya Watahiniwa waliosajiliwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne ilikuwa 538,024, hivyo kuna ongezeko la Watahiniwa 28,816 ambao ni sawa na asilimia 5.36 kwa Mwaka 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.