• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KIJIJI Namtumbo chaingiza milioni 100 kwa uvunaji misitu

Imewekwa kuanzia tarehe: July 11th, 2023

Kijiji Namtumbo chaingiza zaidi ya milioni 100 uvunaji msitu

Kijiji cha Kitanda wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma kimeingiza shilingi milioni 107,115,000 kutokana na uvunaji wa msitu wa hifadhi wa kijiji hicho .

Mtendaji wa kijiji cha kitanda Ayubu Muhuwa alisema kijiji cha kitanda kilipata fedha hiyo kutokana na kuvuna msitu wa hifadhi ya kijiji uitwao Mtaungana wenye ukubwa wa hekta 11,930.

Muhuwa amesema kijiji cha Kitanda kilipata elimu ya mradi wa uhifadhi kutoka MJUMITA,WWF na MCID(MPINGO) kuanzia mwaka 2016 na baada ya hapo walitafuta wavunaji wa magogo kutoka kwenye msitu wao na kujipatia shilingi milioni 107,115,000.

Joseph Kanisius Ngonyani Mwenyekiti wa kijiji cha Kitanda pamoja na kukiri kupokea kiasi hicho cha fedha alifafanua mgawanyo wa fedha hizo kuwa shilingi 62,126,700 zilipelekwa kwa Halmashauri ya kijiji cha kitanda,shilingi 5,355,750 zilipelekwa kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo na shilingi 39,632,550 zilipelekwa kwenye kamati ya maliasili kijiji cha kitanda alifafanua mwenyekiti huyo

Ngonyani alidai kuwa, kupitia mapato yaliyotokana na uvunaji wa msitu huo wa hifadhi kijiji kupitia mgao huo wa shilingi 62,126,700 kilitoa fedha kwa kila shule shilingi milioni 1,280,000 kwa shule 3 za msingi ya Lugongoro, Kitanda na shule ya msingi ya Mkomanile zote za kijiji hicho jumla ya shilingi 3,840,000 kwa ajili ya kutengenezea madawati.

Hata hivyo Ngonyani alidai kupitia fedha hizo pia waliweza kutumia kiasi cha 29,939,500 kujenga jengo la huduma ya mama na mtoto (maternity) baada ya kuwa na hitaji hilo kutoka kwenye zahanati yao ya kijiji na kisha kutumia shilingi 21,371,000 kujenga nyumba mbili za waganga jengo ambalo nalo lipo katika hatua ya ukamilishaji.

Afisa misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Gravas Mwalyombo pamoja na kukipongeza kijiji cha Kitanda kwa kusimamia vyema msitu wa hifadhi ya kijiji, aliwapongeza viongozi na wananchi wa kijiji hicho kwa kutumia pato litokanalo na uvunaji wa misitu kuondoa changamoto zinazowakabili katika kijiji chao.

Mwalyombo alidai maono waliyonayo wananchi na viongozi hao kujenga miundombinu katika kuboresha zahanati yao na kuimarisha elimu kwa kutengeneza madawati ni jambo la kuigwa na viongozi wa vijiji vingine.

Kijiji cha Kitanda ni miongoni mwa vijiji vya wilaya ya Namtumbo venye utajiri mkubwa wa misitu vilivyotengwa na kijiji kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi ambapo kupitia msitu huo waliweza kuvuna magogo yenye jumla ya meta za ujazo (CBM) 369.362. na kuuza na kukipatia shilingi 107,115,000.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.