Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wazazi na walezi kuwajibika katika kujenga malezi ya familia zao lengo ni kuwa na jamii bora ambayo itafuata misingi ya mila na desturi za kitanzania.
Hayo ameyasema katika kilele cha maadhimisho ya siku ya familia duniani ambapo kimkoa yamefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea na kuudhuliwa na Viongizi mbalimbali pamoja na Wananchi.
Kanali Thomas amesema suala ya kukemea mmong’onyoko wa maadili katika familia si la Serikali pekee yake bali ni wajibu wa jamii nzima kutakaza na kukemea viashiria vyote vya tabia mbaya katika familia.
“Maadhimisho haya yana wakumbusha Wazazi na walezi kujukumu lao la msingi la malezi ya watoto na familia zao ni wajibu wa kila mzazi na kila mlezi kusimamia malezi kwa watoto wake katika maeneo makuu matatu ambayo ni kumjali mtoto katika malezi ya msingi, kumlinda mtoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuzungumza na mtoto mara kwa mara ili kufahamu changamoto zinazomkabili”
Maadhimshi hayo ufanyika kila mwaka ifikapo Mei 15, Ambapo kwa mwaka huu 2023 kauli ni “Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia Imara”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.