Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameyataja moja ya maazimio ya kulinda haki za mwanamke ni kutokomeza mila na desturi zinazokandamiza wanawake.
Alikuwa anazungumza kwenye kilele cha siku ya wanawake Duniani ambazo kimkoa zimefanyika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameyata moja ya maazimio ya kulinda haki za mwanamke ni kutokomeza mila na desturi zinazokandamiza wanawake.Alikuwa an azungumza kwenye kilele cha siku ya wanawake Duniani ambazo kimkoa zimefanyika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songeawakumbusha kutokomeza visababishi vya umaskini katika ngazi ya Kaya na kunyimwa haki katika umiliki wa rasilimali ardhi.
‘’Serikali ya awamu ya sita imesimamia kidete katika kulinda haki na kujenga usawa kwa jamii ikiwemo kumiliki ardhi, kumpiga mwanamke, ubakaji, kutelekeza mwanamke na familia”,alisema.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Xzavelia Mlimira amesema siku hii ya wanawake inatumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake na kuongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia.
Akisoma Risala Mwakilishi wa wanawake Mkoa wa Ruvuma Mariamu Juma amesema maadhimisho haya yanakumbusha na kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu hususani wanawake na watoto.
Hata hivyo ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yamejikita katika kauli mbiu inayosaidia kutambua kuwa wanawake na wanaume wanajukumu la pamoja la kuleta maendeleo kwenye jamii kwa kushiriki katika maeneo mbalimbali yakiwepo ya kimaamuzi kuanzia ngazi za kifamilia hadi Taifa.
kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani mwaka 2022 Kizazi cha Haki na usawa kwa Maendeleo Endelevu; Tujitokeze Kuhesabiwa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 9 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.