Hiki ni kisiwa cha Puulu ziwa Nyasa wiayani Nyasa mkoani Ruvuma.Kisiwa hiki kipo Kata ya Liuli kutoka katika fukwe za Puulu hadi ndani ya kisiwa kwa boti ni umbali wa dakika tatu .kisiwa hiki kina vivutio mbalimbali ikiwemo msitu wenye miti ya asili ambayo ni kijani wakati wote,kuna makazi ya ndege adimu duniani wakiwemo ndege aina ya ngwazi wenye uwezo wa kuvua samaki,pia kisiwa hiki ni makazi ya ndege aina ya kanga na samaki watamu wa aina mbalimbali wanazaliana kando kando mwa kisiwa cha Puulu.Kisiwa hiki ni sehemu tulivu ya kupumzika kikiwa ha hali ya ubaridi wakati wote na upepo mwanana kutoka katika ziwa Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.