Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa ameishukuru serikali ya Awamu ya sita kwa kuhakikisha kuwa Tanzania na Mkoa wa Ruvuma unaendelea kufunguka katika Nyanja mbalimbali za usafiri ukiwemo usafiri wa anga.
“Leo nimefika hapa katika uwanja wa ndege wa Songea kukagua kazi ambazo zimekuwa zinaendelea za kukarabati uwanja huu,ikiwemo kuurefusha uwanja na miumbombinu ambayo sasa imewezesha kuongeza ratiba ya safari za ndege kutoka mara mbili kwa wiki hadi mara tatu’’,alisema RC Thomas.
Ametoa rai kwa wananchi mkoani Ruvuma ,mikoa jirani na Nyanda za Juu Kusini kuutumia uwanja wa ndege wa Songea ambao sasa upo tayari kutumika kusafiri kwa haraka ndani ya Tanzania na kuelekea maeneo mengine duniani.
Mkuu wa Mkoa anayakaribisha mashirika mengine ambayo yanaliona soko la usafiri wa anga la Kusini kupitia Songea wafike kwa sababu uwanja wa ndege upo salama na kwamba kiu ya wananchi wa Ruvuma ni kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa haraka zaidi ndani na nje ya nchi kupitia usafiri wa anga.
Hata hivyo Kanali Thomas amesema kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Songea,kuna fungua fursa za uwekezaji na utalii,kwa sababu Mkoa una vivutio vya kila aina likiwemo ziwa Nyasa,Hifadhi ya Taifa ya Nyerere,Mto Ruvuma,milima ya Livingstone na maeneo mengi yenye utalii wa kihistoria na kiutamaduni.
Kwa upande wake Meneja wa Ndege wa Songea Jordan Mchame amesema mara baada ya serikali kukarabati kiwanja cha ndege,idadi ya abiria inazidi kuongezeka ambapo ndege ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiari 76 hivi sasa inabeba abiria kati ya 65 hadi 74.
“Hali hiyo inaonesha kwamba kuna abiria wengi wanaosafiri kwa ndege kwa kutumia uwanja wa ndege wa Songea,usafiri wa anga ni wa haraka na salama kuliko aina nyingine zote za usafiri,kadri idadi ya abiria inavyoongezeka tunatarajia hata gharama za nauli zitapungua’’,alisisitiza Mchami.
Hata hivyo amesema kabla ya ATCL kuanza kutoa huduma,nauli ya ndege binafsi kutoka Songea hadi Dar es salaam kwenda pekee ilikuwa kati ya shilingi 500,000 hadi 600,000 ambapo hivi sasa kupitia ATCL nauli kwenda ni shilingi 250,000 ,ambapo kwenda na kurudi ni shilingi 375,000 tu.
Kiwanja cha ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja bora vya ndege Tanzania ambacho kilijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980 na kiliwekewa lami hivyo kuwa na uwezo wa kutua ndege majira yote masika na kiangazi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.