Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema kupitia Kongamano la Kitaifa la Kisayansi litawasaidia wataalam kafanya mapitio ya tafiti mbalimbali zilizofanyika.
Amesema hayo wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, katika Kongamano la Kitaifa la Kisayansi lililofanyika katika ukumbi wa Chandamali mjini Songea mkoani Ruvuma, kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.
"Kupitia Kongamano hili la Kisayansi ninaamini litasaidia wataalam wetu wa ndani na nje ya mkoa wetu kufanya mapitio ya huduma na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika ili kuweza kutuhabarisha zaidi mbinu bora za kutekeleza afua na utoaji wa huduma bora," Alisema Mhe.Ndile.
Ameongeza kuwa mapitio ya matokeo ya tafiti hizo yatasaidia kuhakikisha ufikiaji wa malengo ya kimkakati ya kudhibiti UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.