Kuelekea tamasha la utamaduni la kitaifa Ruvuma kuanzia Septemba 20 hadi 23 mwaka huu,Wilaya ya Nyasa bado ina fursa za maliasili ya kutosha zikiwemo misitu, wanyamapori, samaki, mito, ziwa, fukwe na mali kale ambazo hazijaharibiwa ndiyo maana tunasema wilaya ya Nyasa ni benki ya vivutio vya utalii na uwekezaji.
Fursa hizo zinaweza kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa na wananchi wa wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla kupitia utalii wa kiutamaduni na ikolojia. Makao makuu ya Wilaya ya Nyasa yapo katika Mji wa Mbambabay.
Wilaya ya Nyasa ina sifa ya kuwepo kwenye bonde la ufa, ambapo bonde hilo huanza kuonekana kutoka katika maeneo ya Buruma, unaposhuka milima katika kona zinazoitwa Ambrosi.
Moja ya kivutio adimu cha utalii katika wilaya ya Nyasa ni uwepo wa Ziwa Nyasa ambalo linapatikana Kusini – Magharibi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani,ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Ziwa hilo lina kina cha kati ya mita 426 na 758 na hii ni kutokana na kupitiwa na bonde la ufa. Kwa upande wa Tanzania mito mingi inapatikana ikitokea wilaya ya Nyasa katika safu za milima ya Livingstone, mito hiyo ni Ruhuhu, Lumeme, Ruhekei, Lwika, Mbamba Bay, Likumbo na Chiwindi ambayo huingiza maji ndani ya Ziwa Nyasa.
Ziwa Nyasa ni kuvutio kikubwa cha Utalii kanda ya kusini kwa kuwa limesheheni vitu vingi ndani yake na tabia tofauti ukilinganisha na maziwa mengine ya hapa nchini na duniani kote.
Baadhi ya tabia za ziwa hili ni uwepo wa maji meupe na maangavu eneo lote la ziwa na mawe marefu ambayo yanajulikana kwa majina ya hia na mala yanayobeba sifa tofauti.
Tabia nyingine za Ziwa hilo ni mawimbi makubwa, fukwe nzuri na zenye sifa tofauti, mawe kuonekana kama sakafu eneo la Chiwindi, fukwe zenye udongo wa mfinyanzi, kina cha maji kuwa kifupi kwa umbali
Ziwa Nyasa ni kuvutio kikubwa cha Utalii kanda ya kusini kwa kuwa limesheheni vitu vingi ndani yake na tabia tofauti ukilinganisha na maziwa mengine ya hapa nchini na duniani kote.
Baadhi ya tabia za ziwa hili ni uwepo wa maji meupe na maangavu eneo lote la ziwa na mawe marefu ambayo yanajulikana kwa majina ya hia na mala yanayobeba sifa tofauti.
Tabia nyingine za Ziwa hilo ni mawimbi makubwa, fukwe nzuri na zenye sifa tofauti, mawe kuonekana kama sakafu eneo la Chiwindi, fukwe zenye udongo wa mfinyanzi, kina cha maji kuwa kifupi kwa umbali.
Kivutio kingine ni msitu wa Mbamba ambapo wenyeji wa Wilaya ya Nyasa, hutumia msitu wa Mbamba kwa matambiko ya kupiga ngoma za kufukuza au kuita majini kwa imani zao na kwamba katika msitu huo kuna wanyama kama chui wakitokea milima ya Nangombo, Ukuli na Chinyemba ambao wanapatikana katika rasi hiyo, wakiwafuata wanyama aina ya ngedere waliopo kwa wingi katika msitu huo.
Maeneo mengine ya vivutio vya utalii kwa Wilaya hiyo anayataja kuwa ni visiwa vya Mbamba, Lundo,Hongi na jiwe la Pomonda ambapo vivutio vyote hivyo vikitangazwa vizuri vitachangia kukuza utalii kwa kuvutia watalii na wawekezaji wa ndani na nje.
Wilaya ya Nyasa pia ina vivutio vya mambokale vingi ambavyo vinapaswa kupewa kipaumbele kwa sababu vinachangia katika kukuza historia na kuendeleza utalii.
Vivutio vya mambokale vimegawanyika katika sehemu ambazo ni historia za mambokale zilizofanywa na viongozi wa nchi katika maeneo mbalimbali na kuingia kwa dini na madhehebu ambayo yameacha alama kubwa.
Baadhi ya vivutio vya mambokale katika wilaya ya Nyasa ni Katika kijiji cha Mbamba bay wakati huo, Rais Mstaafu wa Awamu ya kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Oscar Kambona katika harakati za kudai Uhuru walilala hapo miaka ya 1956 nyumbani kwa dada wa Oscar Kambona ambapo palikuwa na ofisi ya chama cha TANU.
Magavana wa Shirikisho wa Rodesia na Nyasaland walikutana katika (Rest House) katika kijiji cha Mbambabay wakati huo,ambapo jengo ambalo hivi sasa ni ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbambabay wakiwa na lengo la kuagana kutokana na vuguvugu la waafrika kudai Uhuru 1959 kushika kasi. Jengo hilo lilijengwa kwa miti.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.