SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeleta simba wawili majike katika bustani ya wanyamapori Ruhila Manispaa ya Songea
Antony Masebe ni Kamanda wa Kituo Kidogo cha Kanda Kusini Mashariki amesema simba hao wamechukuliwa katika hifadhi moja mkoani Arusha
Ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kuhakikisha katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka wakiwa na familia zao wanafika kufanya utalii wa ndani katika bustani ya Ruhila iliyopo kilometa saba tu kutoka katikati ya mji wa Songea
Amekitaja kiingilio katika bustani hiyo kuwa ni shilingi 2,360 kwa mtu wa kuanzia umri wa miaka 18,chini ya miaka 17 ni shilingi 1180 na kwa Watoto chini ya miaka mitano wanaingia bure.Bustani ya asili ya Ruhila ilianzishwa mwaka 1973
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.