Katikati ya maji ya ziwa Nyasa, ndani ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kunapatikana kisiwa kidogo kinachojulikana kama Kisiwa cha Lundo.
Kisiwa hiki kina ukubwa wa hekta 20 tu, lakini ndani ya eneo hilo dogo, kimebeba historia kubwa inayogusa nyoyo za wengi na kutufunza kuhusu kipindi kigumu cha historia ya Tanganyika.
Lundo si tu kisiwa, bali ni ukumbusho hai wa athari za vita na ukoloni. Baada ya Vita ya Majimaji iliyodumu kati ya mwaka 1905 hadi 1907, wakoloni wa Kijerumani walikifanya kisiwa hiki kuwa sehemu ya kuwahifadhi watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma.
Kuanzia mwaka 1908, wagonjwa wa ukoma walikuwa wakipelekwa katika kisiwa hiki, mbali na jamii zao, kwa lengo la kuwatenga na kuzuia maambukizi, lakini pia kwa sababu ya hofu na unyanyapaa uliokuwa umejengeka dhidi ya ugonjwa huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.