KATIBU Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki ameongoza sherehe za kutimiza miaka 100 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Maadhimisho hayo yameambatana na sherehe za kuaga mwaka 2021 na kukaribisha mwaka 2022 pamoja na kuwaaga watumishi 15 waliostaafu 2021.
Ndaki akihutubia katika Sherehe hizo ametoa rai Madaktari na wauguzi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu pamoja na kuheshima kazi ambayo Serikali imewapa nakuwaamini.
Katibu Tawala amewapongeza wastaafu 15 kwa kazi walizofanya kwa moyo mpaka kufikia miaka ya kuondoka katika utendaji.
“Wastaafu ujuzi wenu mkaendelee kuutumia maana bado tunawahitaji na pia ni watu muhimu sana katika sekta ya Afya”
Mganaga Mkuu wa Hospitali hiyo Magafu Mzigaba katika sherehe hizo amesema hufanyika kila mwaka pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo pamoja na kujikabidhi mikononi mwa Mungu ili aendelee kuwajali katika Kazi wanazofanya.
Mzigaba amewaasa wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa (HOMSO) kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo wa upendo ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma zinazostahili.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Januari 30,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.