MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amefunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria akimwakilisha MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbaert Ibuge.
Akisoma hotuba yake katika Hafla fupi iliyofanyika katika Bustani ya Manispa ya Songea amesema Huduma ya msaada wa Kisheria inasimamiwa na Sheria ya Msaada wa Kisheria Na.1 ya mwaka 2017.
Amesema kauli mbiu ya Mwaka huu 2021 ni Maboresho Endelevu ya Haki jinai katika Kuimarisha upatikanaji wa Haki Jinai, maadhimisho hayo yamekuwa ya kipekee sana yanasisitiza matumizi na uboreshaji wa mfumo mzima wa haki jinai katika sheria zake.
Mgema ameeleza maboresho hayo ikiwemo mbadala wa kifungo na kufanya kazi za kijamii kwa makosa ambayo si makubwa,Mkuu wa kitengo cha Polisi ana mamlaka ya kupunguza adhabu chini ya Sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai kifungu cha 170(6).
Amesema Dhamana ni haki ya mtuhumiwa anaposubiri shauri lake kusikilizwa anaweza kuedelea na majukumu yake ya uzalishaji wa Mali na kuinua uchumi wa Taifa.
Hata hivyo amesema faida za kutumia uangalizi wadola katika mahabusu kusaidia kupunguza mrundikano wa wafungwa na mahabusu katika Magereza nchini ,kupunguza mashauri na kuokoa muda pale mtuhumiwa anapoamriwa kulipa faini Pamoja na kuinua uchumi wanchi mtu akiwa huru anaweza kufanya majukumu yake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kishaeria Mkoa wa Ruvuma Naomi amesema Wizara inalenga kuadhimisha Wiki ya Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kupitia Wasajili wasaidizi wa kutoa huduma ya Msaada wa Kisheria kwa ngazi ya Mkoa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoaka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Novemba 12,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.