I
MWENYEKITI wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru (TAMCU) Mussa Manjaule, ametoa rai kwa maafisa ugani wa chama hicho,kuhakikisha wanakwenda kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo cha kisasa itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao
Manjaule amewashauri wakulima wa zao la korosho,ufuta,mbaazi na mazao mengine yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kujiunga katika vyama vya msingi vya ushirika ili waweze kupata huduma za ugani kwa urahisi.
Manjaule,ametoa ushauri huo wakati akizungumza na wawakilishi wa wakulima,viongozi wa AMCOS na watendaji wa Chama kikuu cha Ushirika(TAMCU LTD)katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa chama hicho mjini Tunduru.
Katika hatua nyingine,Manjaule amewaonya vijana kuacha kukaa vijiweni na kucheza kamali,badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo cha korosho ili waondokane na umaskini.
Afisa Kilimo wa Chama hicho Grace Evody,amewashauri wakulima kutumia mbegu bora zinazostahimii magonjwa na hali ya ukame,badala ya kununua mbegu za mitaani zinazotoa mavuno kidogo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bodi ya Korosho Tanzania(TCB) tawi la Tunduru Samwel Kambona alisema,wameaanza kusajili wakulima wote wa korosho kwa lengo la kuwatambua na kupata idadi kamili wanaostahili kupata pembejeo za ruzuku.
Kambona,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kutoa ruzuku ya asilimia 100 kwa wakulima wa korosho na kusisitiza kuwa,nje ya mfumo huo hakuna mkulima atakayepata viautilifu vya ruzuku.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.