WAKALA wa Misitu Tanzania TFS katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wameanza kutoa elimu ya upandaji miti na faida zake kwa vikundi mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu uhifadhi wa mazingira
Afisa wa Shamba la Miti Wino Saimon Tonoro ametoa elimu ya upandaji miri katika Sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Halamshauri ya Madaba.
Tonoro amesema TFS Wino wanasimamia upandaji Miti na shamaba hilo linajumla ya Hekta 39 na wameligawa katika safu tatu ikiwa safu ya Wino zipo hekta takribani 2,000,safu ya Ifinga hekta 20,000 na Mkongotema.
Amesema shughuli kubwa ambayo TFS wanaifanya ni upandaji miti na utunzaji wa Mazingira pamoja na ufugaji wa nyuki.
Tonoro amesema Serikali imewekeza kwa nguvu kubwa zoezi la upandaji miti na unafaida nyingi ikiwemo utunzaji wa Mazingira,utunzaji wa vyanzo vya Maji,upatikanaji wa nishati ya umeme.
Amesema ukitaka kupanda Miti lazima uandae eneo vizuri kwa kufyeka pamoja na kuzingatia taratibu za uchomaji moto ,na kusubili msimu wa mvua kuanza.
“Hekta Moja inabidi upande miti 1111 kupanda miti mingi ndani ya eneo moja siyo kupata faida miti haita nenepa kwenye hekari 544 miti hadi mti mita 3”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.