MAAFISA UGANI 27 MBINGA WAKABIDHIWA VITENDEAKAZI
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe. Aziza Mangosongo amekabidhi vifaa vya Kilimo kwa maafisa Ugani 27 wa kata zote zilizopo katika Halmashauri ya mji wa Mbinga.
Vifaa vilivyokabidhiwa kwa maafisa ugani hao ni kifaa cha kupima afya ya udongo, bomba za kunyunyizia viwatilifu, kompyuta, printa, lamination mashine, Makoti ya mvua,buti na Kishikwambi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Mkuu wa huyo wa Wilaya amesema,vifaa hivyo vitaongeza tija katika Kilimo ambapo amesisitiza Kilimo ni uti wa mgongo kwa kuwa mahitaji mengi ikiwemo chakula na mavazi yanatokana na Kilimo.
“Naishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Kilimo na kuwapatia vifaa maafisa ugani vitakavyowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wakulima’’,alisema.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mbinga mji Enock Ndunguru amesema kipima udongo hicho kitasaidia kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima ili kujua aina ya udongo na Virutubisho vilivyomo na mazao yanayostawi katika eneo hilo.
Amesema wakulima watapata huduma ya kupimiwa afya ya udongo katika mashamba yao na kupatiwa vyeti bila malipo yoyote kama ilivyoagizwa na serikali.
Maafisa ugani katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma wamepewa vitendeakazi vya kilimo ili kutoa huduma za uhakika za kilimo kwa wakulima
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.