AFISA Elimu Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Kisongo amemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki kufungua mafunzo ya maafisa ugani 34 ya maandalizi ya upimaji wa afya ya udongo .
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kisongo amesema wataalam wa kilimo ngazi ya Kata na vijiji mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza zoezi la upimaji wa udongo litakalofanyika katika vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Ruvuma.
Kisongo ametoa rai kwa maafisa kilimo waliopata mafunzo hayo wakasimamie na kutekeleza kwa weledi zoezi la upimaji wa afya ya udongo kwa ujumla wake hususani katika vijiji vitatu hadi vine kwa kila afisa kilimo.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa pikipiki 7000 kwa maafisa ugani wa Kata na Vijiji kwa nchi nzima,Mkoa wa Ruvuma tumepata pikipiki 282”.
Amesema maafisa ugani wa Kata na Vijiji wa Mkoa wa Ruvuma kila mmoja atapata pikipiki moja na seti ya vifaa vya kutolea huduma za ugani katika zoezi la kutambua afya ya udongo katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.
Mtafiti Mkuu wa Udongo Kutoka TARI –UYOLE Fredrick Mlowe katika mafunzo hayo amesema zoezi hili lipokatika awamu ya tatu ya utekelezaji ikiwemo awamu ya kwanza ilikuwa Mkoa wa Mbeya na Songwe awamu ya pili Rukwa,Mbeya ,Iringa na Morogoro.
Mlowe amesema dhima ya mafunzo haya ni kwaajili ya kujenga uelewa wa afya ya udongo katika kanda na matokokeo yake kushauli makampuni ya uzalishaji wa Mbolea na kutoa mapendekezo ya mazao mbalimbali na kurudi katika tija inayostahili.
Mtafiti wa afya ya udongo amesema matokeo hayo yatakuwa na kazi kumi kuwasaidia wazalishaji wa mbolea watengeneze mbolea inayoendana na hali ya maeneo kulingana na matokeo yaliyopatikana katika upimaji wa afya ya udongo.
Kwa upande wake afisa biashara Mkoa wa Ruvuma Martin Joseph akimwakilisha Katubu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Jeremia Sendoro katika mafunzo hayo amesema baada ya upimaji wa afya ya udongo Mkoa utakuwa na kilimo chenye tija ikiwa Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa wa Kilimo.
Amesema kwa maafisa ugani zoezi la mafunzo hayo ni muhimu ili wakashiriki kusaidia wakulima wa Mkoa wa Ruvuma waweze kujua matumizi sahihi ya mbolea ili waweze kulima kwa tija ikiwa mkoa wa Ruvuma kwa miaka mitatu mfululizo umeongozo kwa mazao ya chakula.
“ Nawaomba maafisa ugani kufanya kazi kwa uadilili kwa maeneo sahihi ,Rais alipokuwa Tabora ameeleza mwaka wa fedha utakaanza julai kilimo ni kipaumbele cha kwanza “.
Amesema kilimo ili kilete tija wataalamu mnatakiwa mfanye vizuri kwenye maeneo yote yanayohusika ikiwa kupima afya ya udongo,matumizi ya mbolea sahihi na kutoa elimu kwa wakulimu”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma
Mei 20,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.