MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge awaonya maafisa ugani kuepuka matumizi mabaya ya pikipiki za Serikali.
Hayo amezungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki 286 kwa maafisa Ugani na Maafisa Ushirika wa Mkoa huo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Ibuge amesema Mkoa wa Ruvuma unategemea Kilimo zaidi ya asilimia 87 kwa wakazi na shughuli hizo kuchangia pato la Taifa na Mkoa.
Amesema shughuli hizo za Kilimo pamoja na uvuvi takwimu ya Taifa ya mwaka 2019 Mkoa umechangia pato la Taifa kwa Mwaka kiasi cha zaidi ya shilingi tilioni nne sawa na wastani wa asilimia 3.8 na Mkoa kushika nafasi ya 10.
“ Rais wa Jamhuri ya Muungano ameona changamoto za Wataalam wa kilimo na ushirika na kutupatia pikipiki 7000 kwa nchi ya Tanzania na vifaa vya upimaji wa udongo kwa maafisa ugani Kata na Vijiji”.
Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Ruvuma umekuwa kinara kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa miaka mitatu mfululizo,uzalishaji huo umetokana na wakulima maeneo makubwa ingawa tija ya uzalishaji katika maeneo kuwa mdogo.
“Mkoa wetu wa Ruvuma tumebahatika kupata Mgao wa Pikipiki 286 tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona changamoto hii na kuwezesha ununuzi wa pikipiki na vitendea kazi vya kilimo kwa maafisa ugani”.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma Pololeti Mgema amesema asimia 75 ya watanzania wanategemea Kilimo.
Mgema amesema Kilimo ni Biashara kikiwa na tija hivyo ametoa rai kwa wataalamu kufanya kazi kwa bidii ikiwa kuacha kukaa katika ofisi na kwenda katika maeneo ya wananchi kuwapatia elimu ili waweze kuzalisha kwa tija.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jackson Mbano
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 14,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.