Vijana, maafisa ugani 50 wameanza kupatiwa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kukuza uzalishaji wa zao la korosho Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Kupitia Mpango wa Jenga kesho iliyo bora (BBT), uliopo wizara ya Kilimo, yanalenga kuwajengea vijana hawa uwezo wa vitendo ili waweze kumsaidia Mkulima wa zao la Korosho kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Maafisa Ugani hao ni sehemu ya Maafisa Ugani na kilimo 500 katika mpango jenga kesho iliyo bora (BBT), Uliopo Wizara ya Kilimo, ambao wamesambazwa katika Mikoa ya Mtwara,Lindi,Ruvuma na Pwani.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Ndg. Milongo Sanga Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru, amewasisitiza vijana hao kutimiza majukumu yao kwa dhati ili kuhakikisha lengo la Taifa la kufikia uzalishaji wa zao la Korosho tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/2026 na tani 1,000,000 ifikapo 2029/2030.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.