MAAZIMIO 12 YA KIKAO CHA TATU CHA SERIKALI MTANDAO KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA KUANZIA TAREHE 8/2/2023 HADI 10/2/2023
Maazimio hayo ndiyo maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa wakuu wa Taasisi na watumishi wa umma nchini wakati anafunga kikao kazi hicho jijini Arusha.
1.Taasisi za Umma ziwajibike kutumia TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali ili kuboresha utendaji kazi wa Taasisi
2.Taasisi za umma zihakikishe zinaendesha shughuli za kawaida za Taasisi kidijitali kama vile uendeshaji wa vikao vya menejimenti,Bodi,Halmashauri na vikao vya mabaraza ya madiwani ili kupunguza matumizi ya karatasi.
3.Kila Taasisi ya umma ihakikishe tovuti ya Taasisi inakuwa na taarifa zilizouhisishwa na zinazoendana na wakati muda wote pia tovuti hizo ziboreshwe ili kuendana na teknolojia ya kisasa.
4.Taasisi za umma zitoe kipaumbele katika masuala ya utafiti na ubunifu kwenye eneo la TEHAMA ili kuibua mifumo ya TEHAMA itakayowezesha Taifa kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda ikiwemo kutenga rasilimali fedha kwa ajili ya ubunifu.
5.EGA kwa kushirikiana na Taasisi za umma iendelee kujenga mifumo shirikishi na mifumo ya kisekta katika jitihada za kupunguza upungufu wa mifumo kwenye utumishi wa umma.
6.Wakuu wa Taasisi za umma wanalazimika kujiunga kwenye mfumo mkuu wa serikali wa kubadilishana taarifa ili kuwezesha mifumo kubadilishana taarifa.
7.Taasisi za umma zinalazimika kuhifadhi mifumo yao kwenye vituo vya kuhifadhi data za serikali vilivyoidhinishwa na Mamlaka ya serikali Mtandao ili kupunguza gharama na kuongeza usalama.
Aidha usalama wa mifumo uliokwishajengwa uendelee kuimarishwa ikiwa ni Pamoja na kuwa na vituo vya kujikinga na majanga
8.Wakuu wa Taasisi za umma wasimamie kikamilifu utekelezaji wa sheria ya mtandao namba kumi ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 hasa uanzishwaji wa Kamati za Uongozi wa TEHAMA na kusimamia utendaji kazi wa Kamati hizo
9.Serikali ianzishe utaratibu wa kuwafanyia upekuzi Pamoja na matamko ya kiapo watumishi wa TEHAMA kwa kuwa wanasimamia mifumo na data nyeti za serikali.
10.Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi iweke mkakati wa kuandaa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu katika kufanya ubunifu kwenye masuala ya serikali mtandao na TEHAMA kwa ujumla.
11.Serikali iwekeze na kuanza kutengeneza vifaa vya TEHAMA hapa nchini
12.Mifumo ya TEHAMA ya serikali inayojengwa iwe endelevu ili kuepuka kubadilisha mifumo mara kwa mara kwa kuwa hadi mfumo kuanza kutumika kunakuwa na uwekezaji mkubwa.
Watumishi wa umma 1600 kutoka mikoa yote nchini walishiriki kikao kazi hicho wakiwemo makatibu Tawala wa mikoa yote,wakuregenzi,wawakilishi kutoka Zanzibar ,wakuu wa Taasisi za serikali na watumishi wengine wa umma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.